Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 12, 2024 alipotembelea Ofisi za Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Makao Makuu kwaajili ya kujitambulisha. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Moren Marwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Moren Marwa akizungumza leo Oktoba 12, 2024 mara baada ya kutembelewa na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi kwaajili ya kujitambulisha katika taasisi hiyo.
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kujenga minara 636 Tanzania nzima katika maeneo ya pembezoni ya miji ili kuunganisha na huduma za mawasiliano.
Hayo yamesemwa na leo Oktoba 12, 2024 na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi alipotembelea Ofisi za TTCL Makao Makuu kwaajili ya kujitambulisha. Amesema kuwa Shirika hilo linajielekeza sehemu zenye changamoto ya huduma ya ili kuhakikisha kwamba wanapeleka huduma kama serikali.
Amesema kuwa wanaendelea kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani Septemba, 2024 aliruhusu kusainiwa kwa mkataba kujenga minara 636 nchi nzima kwaajili ya kupeleka huduma kwa wananchi.
"Niipongeze TTCL na uongozi wake kwa kufanya kazi vizuri na kuona kwamba huduma ya mawasiliano hasa pembezoni mwa miji inafika bila wasiwasi." Amesema
Amesema minara hiyo 636 itaenda kujengwa kwenye maeneo ambayo bado huduma ya mawasiliano haijafika vizuri.
"Tunaamini kwa maelekezo ambayo tumepeana watakwenda kusimamia kazi hii lengo ni kuona mwananchi wa Tanzania yule ambaye yupo pembezoni mwa mji anaweze kufikiwa na huduma za mawasiliano.
Licha ya hayo Kunaminara 757 ambayo wamewapa watoa huduma za mawasiliano, TTCL ilipata minara 200 na minara michache imeweza kuwashwa minara kadhaa inaendelea na utekelezaji, lakini minara ile ambayo bado utekelezaji haujaanza tayari wakandarasi wamepatikana. Lengo ni kuona wakandarasi hao waingie kazini kujenga hii minara kwa wakati ili maeneo yale ambayo yako pembezoni mwa miji iweze kuboreshwa kimawasiliano.
Pia Mhandisi Meryprisca amewapongeza kwa ujenzi wa mkongo wa Mawasiliano wa Taifa nchini zambia, ambao umekuwa kivutio kwa barani Afrika na utatoa huduma kwa nchi sita ambazo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia na Malawi.
Kwa Upande wa Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Moren Marwa amewakaribisha kampuni za mawasiliano, sekta binafsi na sekta za ummanchini kwenda kuhifadhi data katika kituo chao cha data.
Pia ameishukuru Serikali kwa kuiwezesha TTCL ili wawafikie wananchi wote nchini kwa kuwapa huduma za mawasiliano ili kuendana na kasi ya maendeleo na teknolojia
Post A Comment: