Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri akizungumza leo Oktoba 24, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa kufungua semina kwa Wakorea na wafanyabiashara wa Tanzania juu ya kukuza ushirikiano katika sekta za maji, Mafuta, gesi, Madini, viwanda na Kilimo.
Mhandiswi Elias Meela kutoka Tume ya Madini iliyochini ya dawati la TIC akitoa wasilisho katika semina ya kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na Korea.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri akizungumza na Balozi wa korea nchini Tanzania, Eunju Ahn pamoja na wageni wengine kabla ya semina ya kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na Korea, semina iliyofanyika leo Oktoba 24,2024 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri akizungumza na Balozi wa korea nchini Tanzania, Eunju Ahn pamoja na wageni wengine wakiwa kwenye semina ya kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na Korea, semina iliyofanyika leo Oktoba 24,2024 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika Semina iliyoandaliwa na TIC kwaajili ya Kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na Korea.
KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimetoa semina ya Miradi kati ya Tanzania na Korea kwa wakorea waliopo nchini na wengine mtandaoni.
Akizungumza wakati wa semina hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo Oktoba 24,2024. Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri amesema kuwa semina hiyo ina lengo la kuimarisha uhusiano wa kibishara na kubadilishana taarifa na kushirikiana katika sekta muhimu za maji, umeme, mafuta gesi na madini.
Teri amesema kuwa seminahiyo imehusisha ujumbe mbalimbali kutoka serikalini na sekta binafsi ya Korea kukiwa na kampuni zaidi ya 38 za Korea na za biashara 50 za Tanzania ambazo zimeonesha nia ya kushirikiana pamoja katika masuala ya uwekezaji na biashara.
"Kuanzia mwaka 1997 hadi Septemba 2024 Korea, kupitia TIC, imesajili miradi yenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 89.94 (USD) ikiwa na miradi 68 na kutoa ajira 4,997.
Amesema Semina hiyo ilikuwa jukwaa muhimu kwa wadau kutoka mataifa Korea na Tanzania ili kukuza ushirikiano unaoweza kuharakisha ukuaji wa uchumi.
"Tunaweka msisitizo kwa majadiliano ya wazi kati ya maafisa wa serikali, viongozi wa biashara, na wataalam wa sekta mbalimbali ili kushughulikia mabadiliko ya sera na kuunda mazingira bora ya uwekezaji wa kigeni.
Licha ya hayo Teri amewashukuru washiriki wote walioshiriki mtandaoni na waliofika katikaukumbini kwaajili ya kushirikisha uzoefu wao na kujua fursa za uwekezaji ambazo Tanzania inatoa.
"Pamoja, tunaweza kujenga uhusiano wa kiuchumi endelevu ambao utawafaidisha Korea na Tanzania."
Semina hiyo imetolewa na TIC kwa kushirikiano na Ubalozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzania, Shirika la Kukuza Uwekezaji wa Biashara la Korea (KOTRA), Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Mfuko wa Sekta binafsi Tanzania (TPSF), na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA).
Pia katika semina hiyo taasisi nyingine zilitoa mawasilisho ni TANESCO, PPPC, TPDC, NDC na Wizara ya Maji pamoja na NMB ambao ni wadhamini.
Post A Comment: