Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Tanga, Husna Sekiboko, ametoa msaada wa vitimwendo 10 vyenye thamani ya shilingi milioni 5 kwa wanafunzi wenye ulemavu katika shule tatu zilizopo Jijini Tanga.
Shule hizo ni pamoja na Shule ya Sekondari Tanga School, Hotern na Maweni Sekondari zote za jijini Tanga .
Msaada huu unalenga kuboresha usafiri wa wanafunzi hao na kusaidia katika mchakato wa kujifunza.
Sekiboko amesema kuwa msaada huo utawasaidia wanafunzi wenye ulemavu kuondokana na changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwakabiri.
Post A Comment: