Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameridhishwa na utoaji wa huduma ya Maji Mkoani Arusha unaotokana na uwekezaji Mkubwa uliofanywa na serikali ya awamu ya sita akiahidi kusimamia kikamilifu upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi wa mkoa wa Arusha.

Kwenye Ziara ya kukagua miradi na utekelezaji wa utoaji wa huduma ya Maji kwa wananchi leo Oktoba 23, 2024, Mhe. Makonda amempongeza pia Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso kwa umahiri wake katika kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika kupeleka huduma ya maji kwa wananchi kote nchini Tanzania.

Katika hatua nyingine Mhe. Makonda amezitaka mamlaka za Maji mkoani Arusha kuja na mkakati maalum wa kusaidia wananchi wasiokuwa na uwezo, kwa kuwaunganishia huduma ya maji na kuwa na mpango wa ulipaji wa gharama za kuunganishiwa huduma ya maji kwa awamu.







Share To:

Post A Comment: