Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia  Hassan ameipongeza wizara ya madini kwa usimamizi mzuri na  madhubuti wa sekta ya madini unaopelekea ukuaji wa haraka na kuwa kinara katika  kuchangia kwenye Pato la Taifa.

Hayo yameelezwa leo Oktoba 13, 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati akifunga maonesho ya Saba ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita.

Aidha Mh Rais Samia ameeleza katika mikakati ya kuimarisha uchumi wa nchi na upatikanaji wa fedha za kigeni Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetenga kiasi cha shilingi Trilioni moja kwa ajili ya ununuzi wa dhahabu  kutoka kwa wachimbaji.

Rais, Dkt. Samia amesema kwamba  sekta ya madini imekuwa na mchango mkubwa katika kuliingizia taifa fedha za kigeni ambapo kwa mwaka wa fedha 2022\/2023 ilichangia asilimia 56 ya fedha za kigeni.

Sambamba na hapo Rais , Dkt.Samia amesema kiasi cha shilingi 250 zimetengwa kama dhamana ya mikopo zitakazo wawezesha wanunuzi wa dhahabu kupata mtaji.

Rais Dkt. Samia amesema kuwa kwa mwaka wa 2023 mauzo ya madini yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni mbili yaliuzwa katika masoko 44 na vituo mbalimbali vya uuzaji madini  vilivyopo sehemu mbalimbali nchini.

Akielezea kuhusu mwenendo wa biashara ya madini nchini kuanzia mwaka 2019 mpaka septemba 2024 , Dkt.Samia amesema kwa kipindi husika kiasi cha tani 20.8 za dhahabu zenye gharama ya shilingi trilioni 5.2 zimenunuliwa kutoka kwa wachimbaji na wafanyabiashara ya madini nchini.

Dkt.Samia ameeleza serikali inatambua mchango wa asilimia 40 kutoka kwa wachimbaji wadogo nchini, ambapo ametoa leseni 21 kwa vikundi vya Vijana na wanawake  vikiwemo vikundi vya GEWOMA , Ushirika Madirisha na TEWOMA vinavyojihusisha na uchimbaji mdogo.








Share To:

Post A Comment: