WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), kutoka Sekta ya Umma, Profesa Adolf Mkenda, amewahimiza wastaafu wanaopokea pensheni kwenye Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), kujihakiki kama taratibu zinavyoelekeza ili waendelee kupokea pensheni.
Profesa Mkenda ametoa wito huo alipotembelea banda la PSSSF, wakati wa ufunguzi rasmi wa Maadhimisho ya 4 ya Wiki ya Huduma za Fedha kwenye viwanja vya Ruanda-Nzovwe jijini Mbeya, Oktoba 23, 2024.
Aidha, amepongeza huduma zilizokuwa zikitolewa kwenye banda hilo, ambapo yeye mwenyewe alijihakiki kupitia alama za vidole (biometric), huku wanachama wengine wakipatiwa elimu ya matumizi ya PSSSF kidigitali inayomuwezesha mwanachama kupata huduma zote zinazotolewa na Mfuko kupitia simu janja na computer.
Post A Comment: