Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo,akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2025/26 kwenye Kamati ya Bajeti.


Dodoma, Tanzania


Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji (OR-MU), leo imewasilisha mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa taifa wa mwaka 2025/26 kwenye kamati ya Bajeti.

Mpango huo uliyowasilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo aliyeambana na Katibu Mkuu Dkt. Tausi Kida, Menejment ya Ofisi hiyo na Tume ya Mipango, aliweka wazi kuwa mpango huo una maeneo makuu ambayo ni mwenendo wa hali ya Uchumi wa Dunia, Mwenendo wa Uchumi wa Taifa na Mafanikio ya Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa mwaka 2023/2024.



Aidha, Mhe. Prof. Mkumbo alifafanua kuhusu utekelezaji wa Miradi 17 ya kielelezo inayolenga kuleta matokeo katika maeneo ya kipaumbele ambayo imegawanyika katika miundombinu ya Usafiri na Usafirishaji pamoja na Miradi ya kuongeza Uzalishaji viwandani.



Sambamba na mapendekezo ya mpango wa maendeleo Mhe. Prof. Mkumbo, ametoa taarifa fupi kwa kamati ya Bajeti kuhusu Miradi ya maendeleo ambayo serikali inashirikiana na Sekta binafsi mikataba ambayo serikali imeingia na makampuni mbalimbali.



Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Mhe. Oran Njeza (Mb,) kwa niamba ya kamati hiyo ameipongeza Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji kwa wasilisho zuri la Mpango wa Maendeleo ikiwemo taarifa ya ziada kuhusu mwenendo miradi ya maendeleo ambayo serikali inashirikiana na sekta binafsi.



Katika hatua nyingine, Mhe. Prof. Mkumbo amewasilisha taarifa ya utendaji kazi wa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji kwa kipindi cha Aprili hadi Septemba 2024, na Hatua zilizofikiwa kwenye uandaaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2050.



Wakipokea taarifa hiyo wajumbe wa kamati ya Utawala Katiba na Sheria chini ya Uwenyekiti wa Mhe. Florent Laurent Kyombo (Mb,) wamejadili na kupata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali kuhusu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji na Mchakato wa uandishi wa Dira ya Maendeleo 2050.
Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: