Ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT Mkoa wa Mbeya chini ya ufadhili wa Taasisi ya Maryprisca Women Empowerment Foundation (MWEF) umezidi kushika kasi katika kipindi cha wiki moja tangu kuanza msingi hivi sasa umefikia umwagaji zege usawa wa mtambaa panya.
Mkurugenzi wa Maryprisca Women Empowerment Foundation ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema nyumba hiyo inagharimu zaidi ya shilingi milioni sabini.
Mwenyekiti wa MWEF Adam Simbaya ameongoza timu nzima katika zoezi hilo ambapo vijana wa kike na kiume kwa umoja wao wamejitokeza kuhakikisha kazi inafanyika kwa ufanisi mkubwa huku wakiishi na kauli mbiu ya "Twende Tukue Pamoja"
Post A Comment: