Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akizungumza na waalikwa mbalimbali na wanafunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania walioshiriki kwenye uzinduzi wa harambee ya Kwaya ya chuo hicho iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wanafunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu wakati wa uzinduzi wa harambee ya Kwaya ya chuo hicho iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa TPSC, Dkt. Ernest Mabonesho akitoa neno la utangulizi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (hayupo pichani) kabla ya kumkaribisha kuzungumza na waalikwa mbalimbali na wanafunzi wa chuo cha TPSC wakati wa uzinduzi wa harambee ya Kwaya ya chuo hicho iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu wakati wa uzinduzi wa harambee ya Kwaya ya chuo hicho iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akiwa ameshika mfano wa hundi ya fedha iliyochangiwa na ofisi hiyo wakati wa uzinduzi wa harambee ya Kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Wengine ni Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (wa pili kushoto) akipokelewa na Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Nolasco Kipanda (wa kwanza kulia) mara baada ya Naibu Waziri huyo kuwasili Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuzindua harambee ya Kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania. Katikati ni Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Ernest Mabonesho.
Wanakwaya wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania wakiimba wakati wa uzinduzi wa harambee ya kwaya ya chuo hicho uliofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akipokea zawadi ya flashi za baadhi ya Viongozi wa Nchi zenye nyimbo 25 za Kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania wakati wa uzinduzi wa harambee ya kwaya hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akiwashukuru wanakwaya wa Manispaa ya Ubungo mara baada ya kuchangia fedha wakati wa uzinduzi wa harambee ya Kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam.


Na. Veronica Mwafisi-Dar es Salaam


Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu ameipongeza kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kwa kuimba nyimbo zinazobeba uzalendo wa taifa la Tanzania.

Mhe. Sangu ameyasema hayo leo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam wakati akimwakilisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuizindua rasmi kwaya hiyo na kuongoza harambee ili iweze kujiimarisha.

Mhe. Sangu amesema amekuwa asikiliza mara kwa mara nyimbo za kwaya hiyo kwasababu zimekuwa zikielimisha masuala mbalimbali yaliyofanyika katika nchi hii ikiwemo suala ya uzalendo.

“Mimi ni shabiki mkubwa wa kwaya hii kabla hata ya kuteuliwa kuwa Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora kwani licha ya kuburudisha imekuwa ikiimba nyimbo za uzalendo, maadili, historia ya nchi yetu na ikielezea utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanywa na viongozi wa nchi yetu toka awamu ya kwanza mpaka sasa. Mhe. Sangu.

Mhe. Sangu ameongeza kuwa, pamoja na changamoto mbalimbali zinazoikabili kwaya hiyo ikiwemo ukosefu wa studio ya kurekodi na chombo cha usafiri lakini wamekuwa wakishiriki katika matukio mbalimbali na kuweza kutekeleza majukumu yao ya kuburudisha, kuelimisha, kufundisha na kuonya.

Ameupongeza uongozi wa TPSC kwa kuongoza na kuisimiamia vizuri kwaya hiyo ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika matukio mbalimbali yakiwemo ya Serikali.

Katika hatua nyingine Mhe. Sangu amewahimiza wanakwaya na washiriki wengine katika hafla hiyo kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili washiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ndio kipaumbele cha taifa kwa sasa, Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonyesha mfano na kujiandikisha, hivyo nawasihi wote wenye sifa tujiandikishe ili tuchague viongozi wanaofaa kwa muskabali wa taifa letu. Mhe. Sangu amesisitiza.

Awali kabla ya kumkaribisha Naibu waziri Sangu kuzindua kwaya hiyo na kuongoza harambee, Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa TPSC, Dkt. Ernest Mabonesho alisema vijana wa kwaya hiyo wamekuwa wazalendo na waadilifu sana katika kulitumikia taifa licha ya changamoto walizo nazo katika uendeshaji wa kwaya hiyo.

Dkt. Mabonesho ametoa shukrani kwa Viongozi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora kwa miongozo na maelekezo mbalimbali ambayo wamekuwa wakiyatoa katika kuiimarisha kwaya hiyo na kuomba kuendelea kuisadia.
Albam yenye jumla ya nyimbo 25 imezinduliwa na kiasi cha shilingi milioni 123 kimechangwa katika hafla hiyo.
Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: