Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Mkoa wa Mbeya Ndg: Ipyana Samson Njiku amepongeza mwenendo wa Zoezi la Uandikishaji Wananchi katika Daftari la Mpiga Kura kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mkoa wa Mbeya kuwa limefata Utaratibu Stahiki hasa Uhuru na Uwazi. 

Ipyana Njiku ameyasema hayo Leo Wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Mwenendo huo na kudai yeye kama M/kit wa CHAUMMA karidhishwa na Namna Zoezi lilivyoendeshwa. 

"Kwa Mkoa wa Mbeya Zoezi limeenda Vizuri hakuna Changamoto yeyote kubwa tuliyoipokea na hata yale Machache yaliyojitokeza tuliwashauri na Wakayafanyia Kazi haraka" Amesema. 

Kuhusu Ushirikishwaji wa Vyama pinzani katika Shughuli za Maendeleo zinazofanywa na Serikali ya Mkoa wa Mbeya Njiku Amesema Mashirikiano ni Mazuri mara zote wanashauriana na kuelekezana kwa Upendo huku dhamila kubwa ikiwa ni kupambania Maslahi ya Watanzania Hata hivyo amewasihi Vijana kujitokeza kuonesha Uwezo wao katika Kugombea Nafasi Mbalimbali katika Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa huku akiamini kuwa Vijana ndio kundi pekee linaweza kuleta Mabadiriko Chanya katika Jamii.

 Mwisho Ndugu: Ipyana amewashukuru Wananchi Kujitokeza katika Zoezi la Uandikishaji na kuwasihi kujitokeza katika Zoezi la Kupiga Kura kwenye Uchaguzi unaotarajiwa Kufanyika Novemba 27 2024.

Share To:

Post A Comment: