Comredi Daniel Mwangili akizungumza na wazazi pamoja viongozi mbalimbali wakati wa mahafali ya Shule ya Sekondari ya Bread of Life iliyopo Mgera Halmashauri ya Iringa
Comredi Daniel Mwangili akigawa vyeti kwa wahitimu wa shule ya sekondari Bread of life mkoani Iringa 

Na Fredy Mgunda, Iringa.


 Ili kuwapatia watoto elimu bora, Wazazi, walezi  wamehimizwa kuchagua shule zinazo simamia misingi ya malezi, tamaduni, mila, desturi  na maadili ya kitanzania ikiwepo na michezo ambayo ni afya na ajira 

Comredi Daniel Mwangili amesema hayo katika Mahafali ya kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Bread of Life iliyopo Mgera Halmashauri ya Iringa.

Awali  Komredi Mwangili amepongeza mmliki wa shule hiyo Shirika la Daily Bread kwa jitihada za kupambana na adui ujinga, maradhi na umaskini  na kuongeza kuwa kuwekeza katika elimu ni mtaji wa maarifa.

"wanafunzi mnaohitimu, ubongo ni mgodi, kamateni sana elimu mliyopewa ili iwasaidie kufikia mafanikio yenu" 

 Mmiliki wa shule hiyo Askofu Dkt Mpeli Mwaisumbe amempongeza Komredi huyo kwa uzalendo wake wa kutoa vifaa vya michezo  na kuthamini kazi ya melezi inayofanyika kupitia shirika la Daily Bread ikiwa ni  jitihada za kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: