Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala ambaye pia ni Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Msalala Bi. Rose manumba leo Oktoba 18, 2024 amekutana na kufanya kikao na vongozi wa vyama vya Siasa vinavyoshiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Msalala, Katika kikao hicho Rose aliwaeleza viongozi hao mabadiliko ya ratiba ya uchukuaji na urudishaji wa fomu  itakuwa ni tarehe 26 Oktoba 2024 hadi  tarehe  1 Novemba 2024 pamoja na ukomo wa viongozi waliopo madarakani ni Oktoba 19, 2024

Sambamba na hilo Mkurugenzi Rose aliwataka viongozi hao kuhakikisha wanaendelea kutoa hamasa na elimu kwa wanachi ili waweze kujiandikisha kwenye orodha ya daftari la Mpigakura.

Vyama vya Siasa vilivyorishiki kikao hicho ni pamoja na CCM, CHADEMA na CHAUMA  ambapo Viongozi wa vyama hivyo kwa pamoja wamekubaliana kuendelea kutoa hamasa na elimu zaidi kwa Wananchi ili waweze kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye orodha ya daftari la wapiga kura pamoja na kusimamia amani wakati wa zoezi zima la uchaguzi.









Share To:

Post A Comment: