Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Adinan Mpyagila akikabidhi zawadi ya cheti mwanafunzi wa shule ya sekondari Lionja wakati wa mahafali ya 15 ya shule hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Adinan Mpyagila akizungumza na wazazi juu ya umuhimu wa elimu kwa watoto wao pamoja jitihada za serikali kuinua elimu hiyo wilaya ya Nachingwea 


Na Fredy Mgunda, Nachingwea, Lindi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Adinan Mpyagila ametangaza kutatua changamoto ya choo cha walimu hadi kufikia 30/11/2024 ili waalimu waendelee kutoa elimu bora kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Lionja.

Akizungumza wakati wa mahafali ya 15 ya shule ya sekondari Lionja, Mpyagila alisema kuwa walimu wanatakiwa kuwa na choo bora ambacho kitakuwa mbali na choo cha wanafunzi ili kulinda heshima ya mwalimu awapo shuleni na nyumbani.

Kufuatia changamoto hiyo mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Adinan Mpyagila alifanya harambee ya ujenzi wa choo hicho na kufanikiwa kukusanya Kiasi cha shilingi 1,553,950 ambayo itasaidia ujenzi wa hadi kufikia tarehe 30/12024.

Mpyagila aliahidi kutoa mpira, jezi, mafuta,unga wa wangano na sukari kwa wanafunzi wa kidato cha nne ili kuwaongezea morali kufanya vizuri kwenye mitihani ya kidato cha nne itakayofanyika hivi karibuni 

Aliwataka wazazi kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto wao katika kipindi ambapo dunia ipo kwenye mageuzi ya sayansi na teknolojia kwa faida ya familia zao na taifa kwa ujumla na aliwapongeza walimu kwa ufaulu wa asilimia 100 katika matokeo ya kidato cha nne na pili.

Aidha Mpyagila alikumbuka changamoto za shule, ikiwemo ukosefu wa mwalimu wa kike, na aliahidi kuchukua hatua za haraka kutatua tatizo hilo ili wanafunzi wa kike waweze kupata mwalimu anayeweza kutatua changamoto zao.

Katika hatua nyingine mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Adinan Mpyagila aliwasihi wananchi kujitokeza kupiga kura na kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa kuongoza miaka mitano ijayo.
Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

mwangaza wa hbari

Post A Comment: