Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba, amewahimiza wananchi wa wilaya hiyo kujikita zaidi katika lishe bora na kuachana na tabia ya ulaji usiofaa ambao umekuwa ukichangia matatizo mbalimbali ya kiafya.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Nzera, Halmashauri ya Wilaya ya Geita, katika maadhimisho ya Siku ya Lishe Duniani, Komba alisisitiza umuhimu wa kutambua kuwa ulaji usiofaa ni chanzo kikubwa cha magonjwa mengi. Alibainisha kuwa ulaji mbaya hupelekea gharama kubwa za matibabu kwa magonjwa yanayosababishwa na lishe duni.



Mkuu huyo wa wilaya aliendelea kueleza kuwa lishe bora ni msingi wa afya bora kwa familia. Alisema kuwa ukosefu wa lishe bora unaweza kusababisha maradhi ya udumavu, tatizo ambalo limeathiri asilimia 39 ya watoto katika mkoa wa Geita kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni.

Komba alihimiza wananchi kuchukua hatua za makusudi kuhakikisha wanaboresha mlo wao ili kuepuka madhara ya kiafya na kuimarisha ustawi wa jamii kwa ujumla.

Mwisho.

Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

JOEL MADUKA

Post A Comment: