Kamishna Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS),Profesa Dos Santos amewataka wadau wa ufugaji nyuki nchini kutumia fursa za mkutano wa Dunia wa Ufugaji wa Nyuki (Apimondia) unaotarajia kufanyika 2027 kuvutia wawekezaji.

Profesa Dos Santos ameyasema hayo leo wakati wa mbio za Nyuki zilizoshirikisha wanariadha 500 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, Ulaya na Asia zenye urefu wa kilometa 10 na kilometa 21 zitakazofanyika  kwenye viwanja vya General Tyre jijini Arusha.

Amesema utunzaji wa mazingira utawezesha nyuki kuzaliana kwa wingu na kuwezesha uchumi kukua na kutoa rai kwa wananchi kufunga nyuki kwa kutumia mizinga ya nyuki kwani nyuki ni mtaji na mazingira lazima yalindwe

Naye Rais wa Taasisi ya Nyuki Afrika, David Mukomana kutoka Zimbambwe, amesema mbio hizo zimefanyika Arusha kwa lengo la kuweka sawa viungo vya mwili pamoja na kutangaza mkutano wa Dunia wa Ufugaji Nyuki 2027(Apimondia ).

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Woker Bees Africa, ( WBA) Restetuta Lopes Lazarus amesema mbio hizo ni kuelezea umuhimu wa nyuki kwa maisha ya binadamu kutokana na umuhimu wake wanatupatia chakula ,asali ambayo ni  tiba ya magonjwa mbalimbali ikiwemo kuboresha kumbukumbu na hiyo ni fursa kwa wananchi kutunza na kuhifadhi mazingira .

Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Iranghe amesema mkoa wa Arusha unategemea kugawa mzinga ya nyuki  milioni 2 leo katika mbio hizo za Nyuki Marathoni mizinga ya nyuki zaidi ya 20 itagaiwa  kwa makundi mbalimbali.

“Tunataka Arusha iwe na nyuki wengi na dunia kwa ujumla kutokana na utunzaji wa mazingira hivyo mkutano wa Epimondia 2027 utakuwa chachu katika kuleta maendeleo ”

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Arusha Gerald Babu alisema mbio hizo ni chachu ya uhamasishaji wa ufugaji nyuki na kuongeza kuwa mbio hizo ni fursa kwa wafugaji nyuki na watanzania kulinda mazingira.

Awali wanariadha 500 Kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, Ulaya na Asia  watashiriki mbio za nyuki marathoni zenye urefu wa kilometa 10 na kilometa 21 zitakazofanyika Oktoba 26 kwenye Viwanja vya General Tyre Jijini Arusha.

Mbio hizo zimelenga  kuelezea umuhimu wa nyuki kwa maisha ya binadamu kutokana na umuhimu wake wanatupatia chakula ,asali ambayo ni  tiba ya magonjwa mbalimbali ikiwemo kuboresha kumbukumbu na hiyo ni fursa kwa Wananchi kutunza na kuhifadhi mazingira .

Washindi katika mbio hizo Kilomita 21 kutoka JKT kwa muda wa saa 1:18:55 akifuatiwa na Nuru Benedicto akitumia muda wa saa 1:21:59 na wanaume mshindi alikuwa Mathayo Sombi akitumia muda wa 1:6:47.

Share To:

Post A Comment: