Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini Tanzania, TASAF, Ndg. Sherdac Mziray, leo October 2, 2024 ametembelea na kukagua mradi wa wa Ujenzi wa kituo cha Afya cha Kata ya Kipagalo, kilichopo Wilaya ya Makete, pamoja na Ujenzi wa Bwalo la Chakula katika shule ya Sekondari Lupalilo iliyopo kata ya Tandala, wilayani humo.

Akiwa katika Ukaguzi huo, Ndg. Mziray, amepongeza juhudi za Halmashauri ya Wilaya ya Makete, chini ya Mkurugenzi wake, Ndg. William M. Makufwe kwa namna bora ambayo imekuwa ikisiamamia utekelezaji wa miradi hiyo TASAF, nakuahidi kushirikiana na ofisi hiyo endapo watapata changamoto yeyote.

Aidha, Mziray amesema kuwa, licha ya kuwepo kwa changamoto za kimiundombinu pamoja na upatikanaji wa wazabuni, lakini bado halmashauri imefanikiwa kwa kiasi kikubwa, kukamilisha kwa baadhi ya miradi licha kuwepo kwa mingine inayoendelea kutekelezwa, kama vile Ujenzi wa kituo cha Afya Kipagalo.

Kwa Upande wake, Mkurugenzi wa Fedha, TASAF, Ndg. Godwin Mkisi, ameagiza kamati za usimamizi wa miradi ngazi ya Jamii, CMS kuhakikisha, wanaendelea kuwa na ushirikiano huo huo waliouonesha katika utekelezaji wa miradi ya TASAF ili iweze kukamilika mapema kabla ya mvua kuanza.

Naye, Meneja Miradi na  Ajira za Muda na Miundombinu, TASAF, Ndg. Paul Kijazi, amesema kuwa mwezi wa kumi mwishoni, watafanya ziara ya ukaguzi wa mradi wa kituo cha Afya cha Kipagalo kujiridhisha kama umekamilika kwa majengo ya Matatu ya nyumba za watumishi 2 kwa 1, Jengo la mama na Mtoto pamoja na Jengo la matibabu ya nje OPD ili fedha za awamu ya pili ziweze kutolewa.

Sambamba na hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Ngd. William M. Makufwe, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Sukuhu Hassan, kwa kuendelea kuipa fedha za miradi Halmashauri hiyo, na kwamba wao wataendelea kuisimamia kikamilifu ili iweze kuwa mkombozi kwa wakazi wa wilaya ya Makete.

Akishukuru kwa niaba ya Wananchi, Diwani wa Kata ya Kipagalo, Mhe. Nehemia Sanga, amemshukuru Rais wa Tanzania kwa kuendelea kuipa fedha za kutosha Kata hiyo, kupitia Miradi mbalimbali.















Share To:

Post A Comment: