Msimamizi wa uchaguzi Msalala Bi. Rose Manumba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ameendelea kuhamasisha wananchi wote wenye sifa kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari la wapiga kura wa serikali za mitaa..
Manumba amewahamisisha wananchi wa Msalala kwenda kujiandikisha kwenye maeneo wanaoishi ili kuweza kupata fursa ya kuchagua viongozi watakao shirikiana nao kuleta maendeleo.
Amesema pia wapo baadhi ya wananchi ambao wanaamini kuwa vitambulisho vya zamani vinaweza kuwasaidia kupiga kura kitu ambacho ni potofu.
"Ili uweze kupiga kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Serikali Nov 27 2024 ni lazima ujiandikishe kwenye Daftari la Sasa kwa mujibu wa maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi."
Post A Comment: