Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameelekeza mchakato wa uanzishaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Jiji la Dar es salaam uanze mara moja ili kuratibu maendeleo yote yanayofanyika kwenye Halmashauri za Mkoa wa Dar es salaam.

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa barabara katika halmashauri tano za Mkoa wa Dar es salaam leo Oktoba 24, 2024 kwenye viwanja vya Mwengeyanga Manispaa ya Temeke.

Amesema Mkoa wa Dar es salaam unatakiwa kuwa Kioo cha nchi na wageni wote wanapokuja hapa wanatakiwa kuona sura ya Tanzania hivyo inapaswa kuwa na chombo kinachoratibu maendeleo yake na kuhakikisha kuwa mipango yote ya maendeleo inayofanyika na inakua na muunganiko.

Ameongeza kuwa kupitia Mradi wa Uendelezaji wa Jiji ma Dar es salaa awamu ya Pili (DMDP II) kuna miradi mikubwa inayotekelezwa kama ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara na uendelezaji wa bonde la mto msimbazi hivyo miradi mikubwa kama hiyo kwenye halmashauri inahitaji chombo cha kusimamia.

"Hata majiji makubwa duniani yote yanakuwa na ‘Metropolitan City’ na sio halmashauri zinazojitemea kila moja inapangwa kivyake kunatakiwa kuwa na chombo ambacho kinaunganisha jitihada zinazofanywa kwenye halmashauri zote na kuzitaribu ili Jiji husika liweze kukua kwa viwango vya kimataifa."

"Nataka hii Dar es salaam iwe ya viwango na ubora na ukuaji wake uratibiwe kwa taratibu maalunu na sio kukua kiholela tu hii itafanya hadhi ya Dar es salaam isikue haraka na kuwa na hadhi ya kimataifa,"amesema.




Share To:

Post A Comment: