Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amewapongeza madiwani wa halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kurejesha umoja na mshikamano katika kutekeleza shughuli za maendeleo na kutatua changamoto za wananchi.
Waziri Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa ziara yake kwenye Jiji la Arusha leo 04.10.2024 alipokuwa akikagua utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo.
Amesema "Madiwani nyie ndio wenye wananchi hapa na ndio mnawawakilisha wananchi kwenye Baraza la madiwani hivyo mnawajibu wa kushughulikia changamoto mnazoziona kwenye maeneo yenu hivyo tambueni nafasi yenu na msimame kwenye nafasi yenu mtatue changamoto za wananchi."
"Mtu asiwachanganye wala kuwavuruga pangeni mipango ya maendeleo ya wananchi na fedha mnazo tekelezeni miradi mnayoona itapunguza changamoto kwa wananchi wenu, fanyeni kazi wala msibabaike mimi nipo pamoja nanyi,"amesema Mhe. Mchengerwa
Post A Comment: