MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu,akizungumza katika mahafali ya Kidato cha Nne shule ta sekondari Mwau iliyopo Kata ya Manginyi
MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameshiriki mahafali ya Kidato cha Nne shule ta sekondari Mwau iliyopo Kata ya Manginyi na kutoa msaada wa mashine ya kudurufu na Sh.Milioni tatu ya kukarabati ofisi ya Walimu na ununuzi wa samani ili kutatua changamoto walizonazo.
Changamoto ni miongoni mwa changamoto walizozitaja kwenye risala na taarifa iliyosomwa na Mkuu wa shule Mwalimu Robert Simon.
Akizungumza katika mahafali hayo Mtaturu amewapongeza wazazi na walimu kwa kuwasimamia watoto kupata elimu iliyo bora na kuhakikisha wanafunzi wanapata lishe shuleni.
Ametumia nafasi hiyo kuwahakikishia kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan itaendelea kuboresha miundombinu ya shule ili kuweka mazingira mazuri ya kujifunzia.
"Kĺatika miaka mitatu serikali ilileta jumla ya Sh Milioni 245 kwa ajili ya kujenga madarasa matano mapya,maabara za sayansi,vyumba viwili na matundu sita ya vyoo,na tukumbuke kabla ya Mwaka 2020 shule ilikuwa na changamoto kubwa ya vyumba vya madarasa,hivyo Rais wetu amesaidia kutatua changamoto hii,"amesema.
Akieleza mabadiliko mengine ya maendeleo yanayoonekana ni umeme,miradi ya maji,barabara katika Kata ya Mang'onyi.
Akisoma taarifa Mkuu wa Shule hiyo Simon ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia kwa kuwaletea fedha za miradi shuleni hapo na hivyo kuondoa changamoto iliyokuwepo awali na kuboresha mazingira ya kujifunzia.
Amempongeza Mbunge Mtaturu kuwa sauti ya wananchi Bungeni kuomba fedha hatimaye changomoto zimetatuliwa.
Pia amemshukuru kwa kuwapelekea kompyuta mbili na printa moja inayosaidia shughuli za kielimu hapo shuleni.
Changamoto alizoziwasilisha ni uhaba wa nyumba za walimu,kutokuwa na mwalimu wa kike,ukosefu wa mashine ya kudurufu ,ukosefu wa jengo la utawala na samani za ofisi.
Akijibu risala hiyo Mtaturu ameahidi atika kujibu kuzipeleka kunakohusika ili zipatiwe ufumbuzi.
Katika kuhamasiaha ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo aliahidi kumtunuku kila mwanafunzi atakayepata ufaulu wa daraja la kwanza Sh.laki moja na upande wa Walimu zikipatikana daraja la kwanza 10 atawatunuku milion moja.
Amewakumbusha kushiriki zoezi la uandikishaji wa daftari la mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2024.
Mwenyekiti wa bodi amemshukuru Mbunge Mtaturu kwa kuendelea kuwa sauti ya wananchi na kulibadilisha jimbo la Singida Mashariki kimaendeleo kwani kila mahali kuna miradi ya kutosha na hivyo kuahidi kuendelea kumuunga mkono.
#SingidaMashariki#MaendeleoYanayoonekana#TuliahidiTumetekelezaTumewafikia#
Post A Comment: