KAIMU Katibu Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Uvccm, Bulugu Magege, amekitaka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuacha kulinajisi zoezi la uandikishaji wa wapiga kura linaloendelea nchini.


Akizungumza leo, Septemba 16, Jijini Dodoma, alipojiandikisha katika shule ya Dodoma Mlimani, Burugu amewasihi vijana kujitokeza kwa wingi katika mchakato huu muhimu wa kujiandikisha na kupiga kura.

Amesema kitendo cha viongozi wa Chadema kuzuia vijana wenye umri wa miaka 18 kujiandikisha kinawanyima haki zao za msingi na kikatiba.

Amesisitiza kwamba zoezi hili linasimamiwa kwa umahiri na Tamisemi, akionyesha kuridhishwa na idadi kubwa ya vituo vya kujiandikisha vilivyowekwa.

Burugu ameongeza kuwa ni muhimu kwa vijana kutumia fursa hii ili kuweza kushiriki katika mchakato wa kidemokrasia na kuhakikisha sauti zao zinaskika.


Share To:

Post A Comment: