Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza (Sekou Toure) tutatoa huduma za tiba mkoba zijulikanazo kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza na mikoa ya jirani.
Upimaji huu utafanyika kwa watoto na watu wazima tarehe 28/10/2024 - 01/11/2024 saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza (Sekou Toure) iliyopo Isamilo jijini Mwanza.
Aidha kutakuwa na wataalamu wa lishe ambao watatoa elimu ya lishe bora itakayowapa wananchi uelewa na kufuata mtindo bora wa maisha utakaowasaidia kuepukana na magonjwa ya moyo ambayo ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza na yanaweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.
Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapo hapo au kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa.
Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0738 153 160.
“Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”.
Imetolewa na:
Anna Nkinda
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano
Post A Comment: