Katika kuadhimisha siku ya afya ya macho duniani Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya leo imezindua rasmi huduma za kibingwa bobezi za matibabu ya macho kwa Watoto wadogo walio chini ya umri wa miaka 15 ambazo awali wagonjwa walikuwa wakipewa rufaa kwenda kuzipata jijini dare es salaam na Dodoma pamoja na moshi.
Akizungumza katika hotuba yake Ndugu Emmanuel Kayuni, Afisa Utumishi Mkoa na Mgeni Rasmi kwenye Maadhimisho ya siku ya afya ya macho ameeleza kuwa Tanzania inaungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku hii muhimu ya afya ya macho kwa wananchi wake kuhamasisha jitihada za kutokomeza ulemavu wa kutokuona na upungufu wa kuona unaozuilika na kueleza kuwa jicho ni kiungo muhimu sana katika mwili wa mwanadamu hivyo sote tunahitaji macho yenye afya bora ili tuweze kufanya kazi za kila siku kwa ufanisi.
Kayuni ameeleza kuwa Mkoa wa Mbeya una jumla ya vituo vya kutolea huduma za Afya 416 ikiwemo na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na wagonjwa waliotibiwa matatizo ya macho mwaka 2023 walikuwa watoto chini ya miaka 15 wanaume 4,251 na Wanawake 4,927 na kufanya jumla yao kuwa 9,178. Ameongezea pia wagonjwa wa macho wenye miaka zaidi ya 15 wanaume walikuwa 14,609 na wanawake 19,826 huku jumla yao ikiwa ni 34,435 na kufanya idadi ya wagonjwa wote kuwa 43,613. Kati yao wenye shida ya mtoto wa jicho walikuwa, watoto chini ya miaka 15 wagonjwa 101, watu wazima 1,662 sawa na asilimia tisa nukta mbili. (9.2).
Nae Dkt Goldlove Mbwanji Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya ampongeza na kuishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wadau wa macho kuja kuwekeza ndani ya nchi yetu, kwani kwa kufanya hivyo, kumekuwa na urahisi katika kutoa huduma za afya ya macho kwa misaada wanayotoa na kuishukuru Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Huduma za macho kwa muongozo na pia msaada wa kitaalamu katika maandalizi ya maadhimisho haya hadi sasa.
Pia Dkt Mbwanji ameeleza kuwa hospitali itaandaa mafunzo maalumu kwa ajili ya wauguzi kutoka vituo mbalimbali vya afya kimkoa na baadae kikanda ili wanapokuwa kupatia chanjo Watoto hao na kuangalia changamoto mbalimbali pia katika swala Watoto kuwa na matatizo ya makengeza waweze kuwafanyia upimaji wa macho yao ili tatizo hilo liweze kugundundulika mapema na kupewa matibabu stahiki.
Nae Dkt. Barnabas Mshangila, Daktari Bingwa Bobezi wa Macho kwa Watoto na Mkuu wa Idara ya Macho, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya idadi ya Watoto 150 waliokuwa wakipewa rufaa kwenda hospitali kubwa nje ya Mbeya ila kwa sasa huduma hizo zinatolewa hapa hapa Mbeya na kushauri wazazi kuepukana na kwenda kununua dawa kwenye maduka bila kupewa maelekezo na madaktari baada ya uchuguzi kufanyika
Ameeleza kuwa Baadhi ya mafanikio tuliyoyafikia ni pamoja na Elimu juu ya afya ya macho kwa jamii kupitia vituo mbalimbali vya Radio runinga, Huduma mkoba kwa wilaya 3 ambazo ni Kyela, Rungwe na Mbeya mjini. Hadi kufikia leo, jumla ya watoto 250 waliweza kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu mbalimbali ya magonjwa ya macho.
Nae Elizabeth Kishiki, Mratibu wa huduma za watoto shirika la KCCO waishukuru hospitali ya rufaa ya kanda Mbeya kwa utengeneza mfumo wa ushirikiano mzur vilevile kuishauri kuendelea kuwekeza zaidi na kutafuta namna bora ya kufanya manunuzi mazuri ya madawa ya macho.
Post A Comment: