Na Tukuswiga Mwaisumbe,Muheza Tanga
Ni habari zenye simulizi ya mafanikio kwa wanawake na wananchi wa shoroba ya Amani Nilo juu ya kilimo cha mazao ya viungo, Bi Esther John Nzalia kutoka kijiji cha Antakae kata ya Kwezitu ni mwanamke wa mfano ambaye analima na kuchajata mazao haya ya viungo.
Kabla ya ujio wa mradi wa USAID tuhifadhi maliasili anasema katika kijiji chao walilima na kuuza mazao kwa mazoea yasiyo na tija, baada ya ujio wa mradi wamepewa miche na elimu bure wameitumia soko limepaa.
Serikali ni msimamizi wa umma dhidi ya wawekezaji katika Maendeleo ya kilimo, Marekebisho ya kiuchumi yamesababisha kufunguka kwa sekta hiyo kwa uwekezaji binafsi katika uzalishaji na usindikaji na masoko ya kilimo.
Ingawa Ushoroba huu una maeneo mazuri ya uzalishaji, Bi Magreth David ( GPF ORGANICS LTD) anasema uzalishaji na uuzaji wa mazao haya ya viungo bado ni wa chini, anasema kuna ukuaji mkubwa wa mahitaji ya mazao ya viungo duniani ikiwa uzalishaji utakuwa na ubora hasa kilimo kisichotumia mbolea za viwandani.
Uwepo wa wadau hawa wa GPF ORGANICS LTD ni fursa kwa wakazi wa shoroba hii ya Amani Nilo kiweza kupata soko la nje na kuweza kuuza mazao yao kwa bei nzuri na kulima mazao yenye ubora unaozingatia kilimo HAI.
#USAID tuhifadhi maliasili
Post A Comment: