Na.Mwandishi Wetu-Kibaha Pwani
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida Mbaga, amefungua mafunzo elekezi kwa Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Umma, Taasisi na Walaka za Serikali kwa lengo la kuwawezesha Watendaji hao kuwa na utendaji na usimamizi wenye tija na unaodumisha uhusiano mwema kazini.
Dkt. Kida, amefungua mafunzo hayo kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Dkt. Moses Kusiluka , katika shule ya Uongozi ya Julius Nyerere Kibaha, Pwani akisisitiza umuhimu wa kusimamia taasisi hizo kwa tija.
Akisoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Kida ametowa wito kwa Watendaji hao kufanya usimamizi madhubuti wa taasisi zao ili kuwezesha utekelezaji wa majukumu kwa viwango vilivyokusudiwa.
Aidha, amewataka kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya Serikali; kujenga na kuimarisha uwezo wa taasisi na kuendelea kujifunza, Usimamizi madhubuti wa rasilimali watu, rasilimali fedha pamoja na rasilimali nyingine za Serikali zilizowekezwa katika. taasisi wanazozisimamia.
Vile vile, amsesisitiza na kuwataka Wakuu hao kujenga uhusiano wa kiutendaji wenye afya baina yao na watumishi mnaowasimamia ikiwemo Bodi za Wakurugenzi, Wizara Mama pamoja na wadau wengine ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa Taasisi wanazosimamia.
“Mhakikishe mnaimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuongeza uchangiaji katika mfuko mkuu wa Serikali ili kufikia malengo ya Serikali ya Taasisi za umma kuchangia katika bajeti ya Serikali” Amesema Dkt. Kida.
Maeneo mengine aliyotilia mkazo kwa wakuu hao wa taasisi za serikali ni kuimarisha matumizi ya TEHAMA na kuhakikisha mifumo inasomana; Kuimarisha mifumo ya utoaji huduma, na Kujenga maadili mema mahala pa kazi ili kuwezesha utoaji wa huduma bora kwa wateja.
Mafunzo hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Taasisi ya Uongozi na Ofisi ya Msajili wa Hazina na yatadumu kwa siku nne mtawalia, ambapo watoa mada wenye uzoefu wamealikwa wakiwemo wataalamu na viongozi kwa lengo la kubadilishana uzoefu.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida Mbaga,akizungumza wakati akifungua mafunzo elekezi kwa Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Umma, Taasisi na Walaka za Serikali kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Dkt. Moses Kusiluka katika shule ya Uongozi ya Julius Nyerere Kibaha, Pwani akisisitiza umuhimu wa kusimamia taasisi hizo kwa tija.
Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo kwa watendaji wakuu wa Taasisi za Umma mjini Kibaha.
Post A Comment: