SERIKALI imesema kuwa itaendelea kuunga mkono kuhudi za Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) sambamba na kutoa maagizo sita kwa taasisi hiyo kwa ajili ya kuimarisha tafiti zenye matokeo katika kuumba mustakabali wa taifa.


Pia Serikali imeeleza kwamba "ESRF ina uwezo wa kuwa kichochezi chenye nguvu kwa maendeleo ya Tanzania, na wanaweza kusaidia kujenga mustakabali wenye mafanikio na usawa zaidi.

Akizungumza leo Oktoba 21,2024 jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya ESRF, Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango aliyekuwa mgeni rasmi ametumia nafasi hiyo kueleza mchango wa ESRF kwa Serikali na kuahidi Serikali kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanyika kwa maslahi mapana ya Taita.

Dk Mpango alisisitiza umuhimu wa suluhu za utafiti zinazoendeshwa ili kushughulikia changamoto za haraka na kuhakikisha maendeleo endelevu. "ESRF imekuwa mshirika muhimu kwa serikali, ikitoa ufahamu unaotokana na ushahidi ambao umewezesha kuwapo kwa maamuzi yetu ya sera.

"Kazi yao imechanga katika juhudi zetu za kuboresha elimu, huduma za afya, kilimo, na sekta nyingine muhimu,"amesema Dk.Mpango na kuongeza tafiti ambazo zinafanywa na ESRF zimekuwa na tija kubwa katika kuchochea kasi ya maendeleo.

Kuhusu maagizo ,Dk.Mpango ameagiza kuwa na tafiti zenye kuchanganua hatari za kimataifa kwa kutathmini athari za mabadiliko ya teknolojia, kutokuwa na uhakika wa uchumi, mabadiliko ya hali ya hewa, na mvutano wa kisiasa kwenye masuala ya kijamii na kiuchumi.

Maagizo mengine ni namna ya kushughulikia ajira ya vijana kwa kutafiti na kuwasilisha matokeo kwa lengo la kutengeneza mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili vijana wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira na ukosefu wa ujuzi.

Pia kuangalia namna ya kutatuana migogoro ya matumizi ya ardhi,kuangalia jinsi ya kubadilisha mikoa mikavu kwa kuunda fursa mpya za ukuaji na kukuza mabadiliko ya kitamaduni kwa kuhakikisha maadili kama vile usahihi, uaminifu, bidii, na ushirikiano ili kukuza maendeleo.

Makamu wa Rais DK.Mpango ameagiza pia kufanyika kwa utafiti wenye kukuza kutoa majibu kwa usimamizi na uongezaji wa thamani katika sekta ya madini ili kuongeza faida.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Profesa Fortunata Makene, ameainisha mipango ya taasisi hiyo ya kupanua shughuli zake za utafiti na uwezo na kusisitiza kuwa wamejitolea kutoa utafiti wenye ubora wa hali ya juu ambao unajulisha utungaji wa sera na kuchangia maendeleo ya Tanzania.

"Kadiri ESRF inavyoingia katika muongo wa nne, mkutano huu umefanyika kama jukwaa la kutafakari mafanikio yake na kuchora njia ya mbele.ESRF inalenga kuendelea kuchukua jukumu muhimu katika safari ya maendeleo ya Tanzania."

Pia amesema wameyapokea maagizo ya Makamu wa Rais wa kufanya utafiti katika maeneo sita likiwemo eneo la soko la ajira na namna gani vijana wananufaika nalo.

Ameongeza kwamba taasisi hiyo inajivunia katika ushiriki wake kwenye mipango ya Serikali ya maendeleo na kukuza uchumi wa nchi na kusisitiza wataendelea kushirikiana na wadau wao, Serikali na vyuo vikuu mbambali vya ndani na nje ya nchi ili kusaidia katika kuwajengea uwezo wataalamu wao katika kufanya tafiti zenye tija.






Share To:

Post A Comment: