Mkurugenzi Msalala Rose Manumba ameawataka wataalam wa Halmashauri ya Msalala kuongeza weredi katika kuwatumikia wanachi ndani ya maeneo yao ya kazi.
DED Manumba ameyasema hayo alipofanya kikao kazi na wataalamu kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala ambapo aliwasisitiza kuongeza juhudi na kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao katika maeneo yao ya kazi sambamba na kusimamia miradi inayo anzishwa kwa fedha za Serikali.
Sanjari na hilo pia aliwataka wataalamu hao kuwa mfano katika maeneo yao kwa kuhakikisha wanajiandikisha katika daftari la mpigakura Serikali za Mitaa na kutoa elimu juu ya umuhimu wa kujiandikisha kwa jamii inayo wazunguka.
Post A Comment: