Na John Walter -Babati 

Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda leo Oktoba 15, 2024 amelazimika kutumia usafiri wa pikipiki na bajaji  kuhamasisha wananchi wa Wilaya ya Babati kujitokeza kushiriki kujiandikisha na kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27, 2024.

Mhe. Kaganda akiwa kwenye bajaji alizunguka maeneo kadhaa ya mji wa Babati ikiwa ni pamoja na kwenye vituo vya maafisa usafirishaji  (bodaboda) na maeneo ya Wamachinga na mama lishe kuwaambia umuhimu wa kujiandikisha kwenye daftari hilo la makazi kwa ajili ya kuchagua wenyeviti wa Mitaa,vijiji na vitongoji. 



Kaganda ambaye naye amejiandikisha katika mtaa wake wa Mrara Mjini Babati amesema zoezi hilo linatumia dakika Moja Hadi mbili kukamilika na kwamba hakuna chochote anapaswa kwenda nacho mtu kituoni , "kikubwa ni kutaja majina yako matatu na kuweka Saini inakuwa umemaliza" alisema Kaganda 


Baadhi ya Wakazi wa mji wa Babati wamempongeza mkuu wa wilaya kwa uhamasishaji huo anaoendelea kuufanya kwa kuwa unawapa msukumo watu kwenda kujiandikisha kwani wengi wao walikuwa wakiufananisha mchakato huo na ule uliopita wa kujiandikisha kwenye daftari la Kudumu la wapiga kura linalosimamiwa na tume huru ya uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi ujao wa madiwani,wabunge na Rais.

Mwenyekiti wa boda boda mkoa wa Manyara Adamu Omari, amesema wataendelea kuhasishana wenyewe kwa wenyewe kwenye vijiwe vyao kwenda kujiandikisha.

Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: