Na. Scola Malinga, WF, Dar es Salaam

Naibu waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) ameipongeza Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa kuandaa mbio za marathon kwa lengo la kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu na kuitangaza Taasisi.


Mhe. Chande ametoa pongezi hizo jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha TIA marathon 2024 ambapo alikuwa mgeni rasmi


“Michezo ikiwemo riadha ni nyenzo muhimu ya kuunganisha watu na kujenga umoja, napenda kuipongeza TIA na wadau wengine kwa kuwezesha jambo hili kufanikiwa ikiwa ni pamoja kushirikisha wadau mbalimbali”, alisema Mhe. Chande.
.
Alisema kuwa michezo inadumisha umoja lakini pia inatoa mwanga kwa vijana wanaopenda michezo na kuimarisha mwili


Aidha amesema kuwa TIA inatekeleza Sera ya Taifa ya maendeleo ya Michezo ya mwaka 1995 ya kuhamasisha wananchi kushiriki michezo na mazoezi ya viungo vya mwili ili kuimarisha afya zao.


Mhe. Chande alisema kuwa pia ibara ya 242 na 243 (c) za Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, CCM 2020-2025, michezo imepewa kipaumbele kikubwa kwa kuwa ni fursa ya ajira, burudani, afya na inawajengea umoja wananchi.


“Kipekee kabisa ninajivunia sana kuona tukio hili likiandaliwa na TIA, taasisi iliyo chini ya wizara ninayoiongoza kwa kauli mbiu yenye nguvu “Run, Inspire, and Support”, alieleza Mhe. Chande.

Alisema Kauli mbiu hiyo inakumbusha umuhimu wa kushiriki kama jamii kwa kusaidia na kuinua wale wenye mahitaji maalumu.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu, Prof. William Amos Pallangyo, alimshukuru Mhe. Chande kwa kuhudhuria mbio za marathon na pia alifananua kuwa michango  mbalimbali ya kifedha kupitia washiriki na wadhamini itatumika kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum, wanawake na vijana ili kufikia malengo yao.

Alisema kuwa  mbio hizo pamoja na mabo mengine zinahamasisjha jamii kushiriki katika uchanguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba 2024.

Share To:

Post A Comment: