Na;Jusline Marco;Arusha
Katibu wa Siasa Wenezi na Mafunzo Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Saipulani Ramsey ameipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuhakikisha Watanzania wanapata haki yao ya msingi ya kuchagua kiongozi wanaomtaka na hiyo ikiwa chini ya ibara ya 8 ibara ndogo ya 1 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa kila baada ya miaka 5 kutakuwa kunafanyika uchaguzi.
Saigulani ametoa pongezi hizo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chama hicho jijini Arusha kuhusiana na hali ya uchaguzi wa serikali za mtaa, namna unavyoenda na mafanikio yaliyopatikana.
Amesema katika Mkoa wa Arusha Chama cha Mapinduzi kimefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 94.8 kwenye suala la uandikishaji kutokana na Mikakati madhubuti yakudumu iliyonayo ya kuingiza wanachama wapya,wafuasi wakereketwa na wenye mapenzi mema na chama hicho kisha kuweza kuwahamasisha kujiandikisha.
"Katika idadi hiyo chama cha mapinduzi kimeshiriki kama mdau, kama vyama vingine vilivyoshiriki na tunawapongeza wananchi wa mkoa wa Arusha kwa kujitokeza na kujiandikisha kwenye daftari la makazi ili kuweza kupata nafasi ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mtaa."
Pamoja na hayo Katibu huyo wa Siasa na uenezi ameeleza kusikitishwa na malalamiko ya Ndg.Godbless Lema aliyoyatoa akidai watu ni wachache na mchakato wa uandikishaji haujakaa sawa ilihali uandikishaji unaenda vizuri, hivyo amewataka wanasiasa kujikitika kuhamasisha wananchi kujiandikisha badala ya kutumia muda wao kutoa malalamiko yasiyofaa.
Akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kanda ya Kaskazini Gobless Lema zilizokuwa zinahusu uchaguzi wa serikali za mtaa katika jiji la Arusha na Mkoa kwa ujumla, Ramsey amesema uchaguzi ni hati miliki ya watanzania wote na wadau wake wakubwa ni vyama vya siasa na serikali inakuwa msimamizi wa uchaguzi.
"Uchaguzi ni vita vya maneno, hoja na mikakati,sasa nimeshazijua hoja za Chadema ni kulialia na mikakati yake ni kutaka kuacha kushiriki michakato ya uandikishaji na kukikafanya chama hicho kutoenenda na yale yaliyoasisiwa kwa malengo yao, chama chochote duniani cha siasa kinaanzishwa kwa sababu ya kushinda uchaguzi na kuunda serikali,sasa Lema anawanyima wanachama wao kushiriki uchaguzi."
"Wananchi, sisi kama Chama tumejitahidi kwa kadri ya uwezo wetu mtaji ambao tulikuwa tumeuhamasisha,tumeuandaa kwa muda mrefu umeleta matokeo makubwa kwa wananachi na tunayo imani kubwa kwamba chama hiki kitaenda kushinda uchaguzi huu ."
"Siisi Chama cha mapinduzi hoja zetu kwenye uchaguzi huu ni mambo tuliyoyafanya kwenye miaka mitano iliyopita,na hayo tutapimwa nayo kwa kuwaambia wananchi kwanini watupe tena nafasi,na mikakati yetu ni kuhakikisha jeshi ambalo lipo ndani ya CCM linatoka na kwenda kuhakikisha chama hiki kinashinda chaguzi na kinaunda serikali."
Ameongeza kuwa uchaguzi wa mwaka huu walianza kuufanya kuanzia mwaka 2019 katika uchaguzi wa serikali za mitaa,vijijj na vitongoji ulipomalizika kwa kuwaandaa wanachama na wagombea wenye sifa.
Amewasihi wakazi wa jiji la Arusha kuwa katika Kara 156, Mitaa 154 ,Vijiji 393 na Vitongoji 1503 watasimamisha wagombea ambao wataweza kuhimili msukumo wa kuleta maendeleo kwenye maeneo yote na wenye ubora wa kuhakikisha wanaendana na kasi ya Rais Dkt.Samia huku mataraijio yao yakiwa ni kuleta viongozi bora.
Post A Comment: