Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati wameandaa Jukwaa la majadiliano  kuhusu nishati safi ya kupikia kwenye bara la Afrika ambapo limefanyika jijini Dar es Salaam katika hotel ya Hayyat.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko  kwenye uzinduzi wa mkutano wa 9 wa soko la Nishati Afrika amesema ifikapo mwaka 2030 wanatarajia takribani watu million 300 wawe wamefikiwa na nishati ya umeme bara la Afrika.

Amesema kuwa, lengo la mkutano huo ni kwenda kujadili na kufanya tafakuri kubwa kama bara juu ya upatikanaji wa Nishati safi ya kupikia ambapo mfumo wake unachangamoto nyingi kwenye utekelezaji wake ikiwemo gharama ya upatikanaji.

"Watu wengi wanalalamika gharama ni kubwa ya kupata huduma hiyo, sasa ni lazima kueka mikakati mizuri ili kuhakikisha gharama za upatikanaji wake uwe rahisi na watu waweze kumudu, ambapo mitungi ya gesi laki 4 itauzwa kwa nusu bei"amesema

Aidha, amesema mkutano huo pamoja na mambo mengine utakua ni maandalizi ya mkutano wa wakuu wa nchi wa Afrika wanaokwenda kujadili masuala ya nishati kwenye bara la Afrika kwani watu 300 sio kazi  rahisi kuwapata. 

Amesema kuwa, Benki ya maendeleo ya Afrika imepima kwa vipimo vyake kwa kukaa na wadau wote ambao wanapata pesa kutoka kwao imeonekana Tanzania imepiga hatua kuwa san na wamefanikiwa jambo lililopelekea nchi hiyo kuwa shamba darasa kwa wenzao kwenye usimamizi wa Sekta ya nishati.

Aidha, amesema nchi Tanzania imepata heshima ambayo haikua kazi rahisi bali Kwa mausiano mazuri ya kidiplimasia kati ya nchi hiyo na Benki ya maendeleo ya Afrika ambapo wamekiri Tanzania imepiga hatua kubwa kwenye masuala ya kisera na usimamizi, uzalishaji na usafirishaji na upelekaji wa umeme Vijijini.

Kwa upande wake, Makamo Mwenyekiti wa Nishati, mabadiliko ya tabia nchi na ukuaji wa kijani AFDB Dr Kevin kairuki wameamua kufanya kazi Kwa pamoja na Tanzania kwa sababu ipo mstari wa mbele katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

"Tanzania imekua ikitilia manani mambo ya nishati safi ndio sababu tukakaa na wadau kama vile World Benki tukasema hili kongamano lifanyike Tanzania kwani kupata watu million 300 wa kutumia nishati safi ya kupikia sio rahisi" amesema Dr Kairuki.

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Eng Felchesmi Mrama amesema mkutano huo wataweza kujadiliana ukuaji wa Nishati, matarajio, namna ya kuipata uzalishaji na ujumuishaji wa Sekta binafsi kwani ifikapo 2034 nishati ipatikane kwa unafuu.











Share To:

Post A Comment: