Na Denis Chambi, Tanga.
BANDARI ya Tanga inajivunia kuvunja rekodi ya ukusanyaji wa mapato ambapo imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi Billion 18.6 kwa kipindi cha July hadi September 2024 huku ikimtaja kampuni ya Sea front kama mteja wake Mkuu ambaye amechangia kwa asilimia 8 kuongezeka kwa pato hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania 'TPA' Afisa uhusiano wa mamalaka hiyo Enock Bwigane wakati wa kupokea Meli iliyobeba shehena ya mizigo mbalimbali kutoka China ikiwemo magari zaidi ya 350 Henock Mwigane amesema kuwa uwekezaji uliofanywa na Serikali katika bandari ya Tanga umefungua milango kwa wafanyabiashara kuanza kuitumia bandari hiyo.
"Tunamshukuru sana mdau wetu kampuni ya Seefront Shipping line ambaye amefanikisha kufika kwa Meli hii ambayo ina shehena mchanganyiko yakiwemo magari zaidi ya 350 na asilimia kubwa ya mizigo inaelekea nje ya nchi kuna shehena ya ndani na ambayo inatoka"
"Kuwepo kwa Meli hii ambayo inahudumiwa siku ya leo kunafikisha idadi ya meli 12 ambazo zimehudumiwa na mteja wetu Seefront ambaye alikuwa akifanya huduma za kibandari katika bandari ya Dar es salaam , uwekezaji uliofanywa na Serikali wa Billion 429.1 kwa awamu zote mbili zote mbili kuboresha bandari ya Tanga kumewezesha meli kubwa zihudumiwe katika bandari hii" alisema Mwigane
"Tunapoongelea ufanisi katika bandari ya Tanga tujivunia katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha ambapo bandari ya Tanga imekusanya mapato ya shilingi Billion 18.6 shilingi Billion 8 zimetokana na mteja huyo, tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa maamuzi yake ya kufanya maboresho katika bandari zote ikiwemo bandari ya Tanga"
Alisema kuwa maboresho yaliyofanyika katika bandari zote hapa nchini yamechochea ufanisi Kwa kiasi kikubwa na kuweza kuchangia pato la Taifa ambapo katika bandari ya Tanga kwa kipindi cha miaka miwili wameweza kuhudumia shehena tani Milion 1.1 kwa mwaka huu wakitarajia kuhudumia shehena ya tani Milion 1.4 ambapo hadi sasa tayari zimeshahudumiwa tani laki 3.3.
"Uwekezaji makubwa uliofanyika katika bandari ya Tanga umepelekea ufanisi kuongezeka, mapato yameongezeka lakini pia huduma ya shehena imeongezeka ukiangalia kwa miaka miwili iliyopita kutoka kuhudumia shehena tani laki 8 tunasogea sasa hivi tuna shehena tani Milion 1.1 mwaka huu tunategemea kuhudumia shehena ya tani Milion 1.4 tunapiga hatua kubwa kwenye kuhudumia shehena nyingi katika bandari ya Tanga
Aidha aliongeza kuwa kupitia bandari ya Tanga nchi mbalimbali zikiwemo Congo ,Zambia na Rwanda zimekuwa zikipitisha mizigo yake hatua ambayo inazidi kuipaisha Tanzania kimataifa.
Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha amesema kuwa hapo awali kulikuwa na baadhi ya bidhaa ambazo zimekuwa hazisafirishwi kupitia bandari hiyo lakini sasa baada ya maboresho yaliyofanyika yakiwemo ya upanuzi wa kina cha bahari na ujenzi wa gati yamekwenda kufungua milango kwa wafanyabiashara kuanza kuitumia Bandari hiyo.
"Maboresho haya yameleta manufaa makubwa kuna baadhi ya bidhaa ambazo zilikuwa hazipiti kabisa katika bandari yetu ya Tanga ikiwemo Copper,Ammonium Nitrate hazijawahi kupita kipindi cha nyuma lakini sasa baada ya maboresho tunaweza kuhudumia tani elfu 41 ya Amonium, tumeweza kuhudumia shehena ya Sulphur tani 104".alisema Mrisha.
Meneja huyo alisema kuwa bandari hiyo yenye ukubwa wa hekta 17 pamoja na uwepo wa maeneo ya Mwambani na Chongoleani wamefanikiwa kutatua changamoto ya uhaba wa maeneo ya kutosha kwaajili ya kuhifadhia shehena ambazo wanazihudumia katika Bandari tofauti na hapo awali.
"Bandari yetu ya Tanga ina ukubwa wa hekta 17 lakini pia tuna eneo la Mwambani lenye ukubwa wa hekta 174, tunalo eneo ambalo kunajengwa Bomba la mafuta ghafila EACOP hekta 207 kwahiyo tumeweza kuondoa tatizo la ufinyu wa eneo ambalo tumekuwa tukizidiwa hapo awali" aliongeza.
Aliongeza kuwa uwekezaji uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan wa kuboresha bandari hiyo haujaleta tu manufaa kwa Serikali bali wananchi hususani wazawa wa Tanga wamekuwa wakinufaika kwa kupata ajira hatua ambayo unakwenda kuinua kipato chao.
Afisa uhusiano wa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania 'TPA' Enock Mwigane akizungumza na waandishi wa habari katika Babdari ya Tanga october 22,2024 kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa mamalaka hiyo.
Post A Comment: