Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa ya pembezoni mwa nchi na mipakani kuimarisha zaidi ulinzi na usalama wa mipaka ili kujilinda na Homa ya nyani ‘Mpox’ kuweza kuingia nchini.
Mhe. Mchengerwa ametoa maagizo hayo leo Jumatano Septemba 18, 2024 wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani Longido mkoani Arusha akitahadharisha kuchukua hatua na kwa Wilaya na Mikoa itakayozembea na kusababisha ugonjwa huo kuingia nchini Tanzania viongozi wake watachukuliwa hatua.
“Ugonjwa huu hauko mbali,upo jirani tu kwahiyo msingi huu wa kuimarisha ulinzi katika mipaka yetu itatusaidia kutambua yule anayeingia lazima afanyiwe uchunguzi wa kiafya kwa mujibu wa namna taratibu za wizara ya afya walivyotupatia.” Amesema Mchengerwa.
Imarisheni ulinzi katika mipaka yetu ili kudhibiti ugonjwa wa Mpox, kila mgeni lazima apimwe asije kuingiza ugonjwa Tanzania hasa kipindi hiki ambacho tunaelelea kwenye Uchaguzi, na anatakayepelekea ugonjwa huu kuingia nchini kwa uzembe ntamchukulia hatua alisisitiza Mhe. Mchengerwa!
Post A Comment: