Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Madini, Taasisi zake pamoja na Wataalam kutoka Vyuo Vikuu vya Dar es Salaam na Dodoma wanaotarajia kushiriki mafunzo ya muda mfupi  katika Taasisi ya Jiolojia ya  nchini India  waliagwa rasmi Septemba 2, 2024 katika Ofisi za Ubalozi wa India nchini.

Wataalam hao wanatarajiwa kupata mafunzo ya kujengewa uwezo katika  masuala yanayohusu shughuli za utafutaji madini.

Ushiriki wa wataalam katika mafunzo hayo ni matokeo ya ushirikiano kati ya Tanzania na India ambapo  yalichagizwa zaidi kufuatia ziara aliyoifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Hassan nchini humo.

Share To:

Post A Comment: