Wasanii wa tamthilia maarufu ya Mawio nchini Tanzania Gabo,Barnaba na Sarah leo wametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro na kupokewa na Balozi Saidi Yakubu.

Wasanii hao walioongozwa na Gabo wamemuelewa Balozi Yakubu wapo Comoro kwa kuwa tamthilia yao ina mashabiki wengi Comoro na hivyo wameamua kurekodi kipande kidogo kisiwani Ngazidja.

Kwa upande wake Balozi Yakubu aliwapongeza kwa hatua hiyo na kuwaeleza kuwa kufanya hivyo kunaongeza ushirikiano na udugu wa kihistoria wa Tanzania na Comoro hususan kwa kuwa kipande hicho kimeshirikisha wacomoro pia.

Katika mkutano huo,Mwenyekiti wa Watanzania nchini Comoro,Robert Shirima alishiriki.













Share To:

Post A Comment: