Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amewahakikishia wananchi wa Kata za Mnyamani,Vingunguti na Buguruni kuwa Serikali inaendelea kuboresha huduma za kijamii kwa Wakazi hao.
Mhe. Mpogolo ameyabainisha hayo leo Septemba 14, 2024 kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Msikate Tamaa vilivyopo Vingunguti ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.
Akizunguzumza katika Mkutano huo, Mhe. Mpogolo amewaeleza kuwa katika changamoto alizozibaini kwenye Kata za Mnyamani, Buguruni na Vingunguti ni pamoja na uchakavu wa miundombinu mbalimbali, mifereji ya maji taka pamoja na kutotengenezwa kwa bonde la Mto Msimbazi hivyo kuwahakikishia wananchi wa Kata hizo kuwa Serikali inaendelea kuboresha miundombinu na punde kituo cha afya vingunguti kitaanza kuboreshwa kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri.
“Halmashauri yetu imekua ikikusanya mapato mengi na pia tumepokea fedha nyingi kutoka Serikali Kuu kwaajili ya kuboresha huduma za Afya, Elimu na miundombinu, hivyo niwahakikishie hizi changamoto zote za huduma za kijamii zinaenda kuisha kabisa, kwani haiwezekani tukusanye mapato mengi lakini tuwe na hizi changamoto ambazo kama Halmashauri tunaweza kuzitatua.” amesema.
Halikadhalika, amewataka Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari kutumia utaratibu maalumu wa kufanya mitihani wananfunzi na sio kila mara kudai ada za mitihani kwani wana waumiza wazazi wenye kipato cha chini huku akiwasisitiza wazazi kuwa wanafunzi kula chakula ni muhimu hivyo wahakikishe wanachangia ada ya chakula.
Katika hatua nyingine, Mhe. Mpogolo amewataka wananchi wa Kata hizo kujiandikisha kwenye daftari la makazi kwaajili ya kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 Sambamba na Kauli mbiu isemayo "
Post A Comment: