JESHI la polisi limesema kuwa limedhamiria kuboresha huduma zake ikiwa ni pamoja na kubadili fikra juu ya jeshi hilo, kusimamia sheria kikamilifu pamoja na kuimarisha matumizi ya mifumo ya tehama na teknolojia katika utendaji wake
Hayo yameelezwa jijini dar es salaam na Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi ilala Kamishna msaidizi wa polisi Mohamed Makusi wakati akipokea vifaa mbalimbali vya tehama ikiwemo kopyuta na printer (vichapishi) vilivyotolewa na wakalwa wa vipimo tanzania kwa jeshi hilo ili kuliongezea ufanisi wa kiutendaji
Vilevile amesema vifaa hivyo Vitasaidia kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kupunguza muda wa utoaji wa huduma hizo.
“Vitatusaidia kutoa huduma bora za kipolisi kwenye ofisi zetu na pia vitasaidia wao (wananchi) kutopoteza muda mwingi kusubiri huduma za kipolisi katika ofisi zetu za kipolisi mkoa wa ilala” Amesema Makusi.
“Kwenye maadhimiaho ya miaka 60 ya jeshi la polisi kauli mbiu ni huduma bora za kipolisi zitapatikana kwa kubadili fikra, usimamizi wa sheria na matumizi ya tehama, hivyo nyinyi mmeingia kwenye eneo la matumizi ya tehama kwa hiyo tunawashukuru sana” Aliongeza kamanda Makusi.
Kwa upande wake meneja wa wakala wa vipimo mkoa wa ilala Muono Nashon amesema lengo ni kuimarisha utendaji wa jeshi la polisi kwani wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu na jeshi hilo kwani kupitia kesi mbalimbali za jinai zinazoibuliwa na wakala wa vipimo.
“Tumekuwa tukifanya kazi kwa karibu sana na jeshi la polisi kwani ukiangalia kazi zetu nyingi zinaendana na jinai ambapo mara nyingi tunawahitaji polisi ili kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake hivyo vifaa hivi vitasaida kuboresha utendaji kazi na kuomarisha mahusiano yetu na jeshi la polisi” Alibainisha Muono
Post A Comment: