CHAMA cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO SACCOS),kimetoa mashuka ya vitanda zaidi ya 1000 kwa lengo la kuboresha hali na faraja kwa wagonjwa katika Hospitali sita. katika maeneo mbalimbali nchini.

Miongoni mwa hospitali hizo ni pamoja na Mwananyamala,Temeke,Ilala,Njombe,Simiyu na Katavi hii ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha huduma za afya nchini.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam,Katibu Mkuu  wa Wizara ya Afya John Jingu alisema mashuka yaliyotolewa na Tanesco  Saccos ni nyenzo  muhimu katika hospitali nchini ambayo  yanasaidia  kuboresha mazingira ya kazi ikiwemo  huduma kwa  wagonjwa.

Alisema ni jukumu la taasisi,kampuni,mashirika na  jamii kuhakikisha linalinda na kutunza maisha ya wagonjwa  kwa kuhakikisha inawajali na kuwashika mikono kwani sote ni wagonjwa watarajiwa.

 "Sisi wote kama jamii tunajukumu la kuhakikisha tunawezesha kufanya kazi vizuri,Serikali imefanya kazi kubwa na inaendelea kufanya  kazi katika kuhakikisha inaboresha mazingira ya sekta ya Afya hivyo na  sisi tukifanya hivyo ni kwa faida ya wengine na faida yetu kwani sisi wote ni wateja wa hospitali watarajiwao,"alisema na kuongeza

"Hospitali ni sehemu ya wote hivyo tunajukumu kuhakikisha hospitali kuna mazingira mazuri ya kutoa huduma,agenda kubwa ya Rais Samia Suluhu Hassan  kwenye sekta ya afya sasa hivi ni kuendelea kuimarisha ubora wa huduma kwa  Wataalam,Wauguzi na Madaktari hivyo  tunajukumu la kuhakikisha hospitali zinafanya vizuri,"alisema.

Alisema Tanesco Saccos inaendelea kuleta  vifaa vya kuwatia moyo wagonjwa na  ni faida kubwa kwa hospitali  kwa watoa huduma na watu binafsi.Kwa Upande wake  Mtendaji Mkuu wa Tanesco Saccos,Andrea Hilary alisema 

kuna umuhimu mkubwa wa kutoa msaada huo kwa i Afya ni haki ya msingi ya binadamu, na Wizara ya Afya imejitolea kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anapata huduma za matibabu bora. 

"Tanesco SACCOS imeonyesha mfano bora wa uwajibikaji wa kijamii wa kampuni kwa kujitokeza kushughulikia baadhi ya mahitaji ya haraka katika hospitali zetu,Shuka  hizi tulizozikabidhi leo mi safi na zenye faraja  kwa huduma za wagonjwa na kupitia mchango huu utaongeza kwa kiasi kikubwa ubora wa huduma zinazotolewa kwa wagonjwa,"alisema.

Naye Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mwananyamala Dkt.Zavery Beneath  alisema wanafuraha kuwakati ya wanufaika wa msaada kutoka Tanesco Saccoss ambapowamepewa mashuka 200 kama hospitali ambapo itawasaidia kupunguza upungufu wa mashuka kwenye hospitali yao

Alisema kila kitanda kimoja cha mgonjwa kinatakiwa kuwa na mashuka nane yanayozunguka kwani kila wakati utakuta mawili yanatumika,mawili yapo stood,mawili yapo kufuliwa na mawili mengine yapo yanasubiri kutumika wakati wowote.

Alisema msaada huo,wanaamini wamesaidia hospitali kutumia  wagonjwa kwa usahihi na viwango vinavyotakiwa vya wizara ya afya.

Alisema kuna uhitaji katika hospitali hiyo ni mashuka 2400 kwa vitanda 300 ambapo kwa mzunguko kwa siku yanatakiwa mashuka nane mara nyingi hayufikii hiyo idsdi kwa kupewa msaada huu wamesaidia serikali kupunguza uhaba wa mashuka katìka hospitali zao.

 Alisema wao kama  vyama vya ushirika wanaendeshwa na misingi saba duniani kote katika kufanya kazi zao,miongoni mwa  misingi hiyo ni pamoja na kujali jamii kama walivyofanya  Tanesco Saccos.

" Tanesco saccos leo wametimiza huo msingi wa saba kuijali jamii,tukiwa katika kampuni au taasisi wanaita CRS ila sisi ni tofauti kwamaana tunaijali na kuigusa jamii kwa  kuangalia jamii inachangamoto gani na kuwasaidia moja kwa moja,"alisema.



Share To:

Post A Comment: