WITO umetolewa kwa sekta binafsi, taasisi za elimu, na mashirika yasiyo ya kiserikali kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wanaandaa vizazi vijavyo kwa uchumi wa akili bandia yani Artificial intelligence(AI).
Wito huo umetolewa leo Septemba 26,2024 jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) wakati akifungua mkutano wa Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT)
Mhandisi Mahundi amesema, Serikali ipo tayari kushirikiana na wadau wote kuhakikisha kuwa wanafanya matumizi bora ya teknolojia za (AI) ili kuboresha maisha ya Watanzania na kuimarisha uchumi wa nchi.
"Tunahitaji kuwekeza katika mafunzo ya kitaaluma na kujenga uwezo wa wafanyakazi wetu ili kuhakikisha kuwa Tanzania ina nafasi nzuri ya kufaidika na mapinduzi haya ya kidijitali,
"Kwa pamoja, tunaweza kufanya mabadiliko haya ya kidijitali kuwa kichocheo cha maendeleo endelevu na ustawi wa taifa letu, ni matumaini yangu kuwa matokeo ya tukio la leo yatatusaidia kuweka msingi mzuri wa uongozi wa kidijitali nchini" amesema Mhandisi Mahundi
Post A Comment: