Na Denis Chambi, Tanga.

MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Buriani ameitaka Hospital ya rufaa ya mkoa  Bombo kuwa ya  mfano kwa kuchukua tahadhari ya kujikinga na na ugonjwa wa Homa ya nyani 'Mpox' ambao  licha ya kutokuwepo hapa nchini bado tahadhari ni lazima zichukuliwe ili kujiweka tayari Kupambana kabla na baada ya kutoka.

Dkt Buriani ameota Rai hiyo wakati alipofanya ziara ya kukagua  na kutembelea maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa katika hospital hiyo kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma ambapo pia  kamati ya usalama ya mkoa ilikabidhi bango linaloonyesha tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo huku akigiza jitihada zilizofanyika wakati wa janga la  COVID-19  zifanyike ili kujikinga.

Amesema kuwa ugonjwa huo ambao kwa sasa umesharipotiwa katika nchi za Kenya ,Uganda pamoja na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo  ni lazima tahadhari zichukuliwe ikizingatiwa kuwa Mkoa wa Tanga upo jirani pamoja na muingiliano wa watu kutoka Kenya wanaokuja Tanzania  katika nyanja mbalimbali ikiwemo za kibiashara.

"Tuna changamoto ya  homa ya nyani 'Mpox' tulifikiri katika hospital ya kwqnza kabisa ya mkoa  ndio muwe kielelezo  sijaona hata mabango mliyoyaweka ya kuonyesha tahadhari ya Empox, sasa hivi kama Empox ipo Kenya ,Uganda, Congo kufika Tanzania sio shida tutaweza tu kuokoka kama tutazingatia masharti ya kujikinga na ugonjwa huu ikiwemo maswala ya kurudi kule tulikofanya wakati wa COVID-19 kuweza kunawa mikono kwa maji tiririka na kutokushikana mikono ili kuepukana na ugonjwa huu" amesema Dkt Buriani

"Sisi kama kamati ya usalama ya mkoa  tumekuja na kielelezo tusisubiri mpaka wizara ituambie cha kufanya , sisi wenyewe tuonyeshe utayari na nyinyi wenyewe kama  mkionyesha wa wilaya vituo vya afya na Zahanati wataiga kila mtu ataenda kuhakikisha hili janga linasimamiwa" alisisitiza.

Aidha Balozi Buriani amesema kutokana na uwepo wa ugonjwa wa kipindipindu ulioibuka katika wilaya ya Kilindi ambapo wagonjwa 88 waliripotiwa zilifanyika jitihada za makusudi ikiwepo timu ya wataalam kuweka Kambi ambapo ilifanikiwa  kupunguza maambukizi hayo hulu Serikali ikiendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuhakikisha inabiresha huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama.

"Tuna changamoto ya kipindipindu kinaendelea kuisha na sasa kipo kwenye wilaya yetu ya Kilindi tulikuwa tuna wagonjwa 88 ndani ya wiki moja tuliagiza wataalamu waweke Kambi wahakikishe kwamba  kusiyokee mgonjwa mwingine tena na sasa leo (Jana) nimeambiwa amebaki mgonjwa mmoja.

"hii imetokana na vyanzo vya maji kutokuwa salama wenzetu wa Kilindi wanategemea sana maji ya Kisima na chem chem tunayo miradi mikubwa ya maji ambayo inaendelea kukamilishwa  mpaka ikifika mwakani tutakuwa tumefikia asilimia 95 ya miradi iliyokamilika mjini na vijijini itakuwa ni 85 na sasa hivi wastani wa upatikanaji wa maji katika Mkoa wetu ni asilimia 56 na maen o kama ya Handeni Kilindi bado ipo chini ya asilimia 40 kwahiyo ikitokea changamoto kama hii ya kipindipindu ni lazima tufanye jitihada zote  tupate madawa ya kuhakikisha tunasafisha yale maji ili mtu ambaye atashindwa kuchemsha awe anapata maji ambayo yameshasafishwa kupitia zile  na hicho ndicho tulichokifanya kupitia kwa mganga Mkuu wa Mkoa lakini tunaendelea kuboresha upatikanaji wa maji katika maeneo yetu ya Handeni  ili kipindipindu kisiendelee kusambaa"

Aidha Dkt Buriani ameipongeza Hospital hiyo kwa kuendelea kutoka huduma kwa wagonjwa licha ya baadhi yao kukosa fedha za matibabu ambapo mpango uliopo sasa ni kuhakikisha wagonjwa wote wanaogika hospitalni hapo wanapatiwa huduma huku wakie delea kulipa kidogo kidogo mpaka deni litakapoisha. 

"Nafurahi kwamba hamzuii wagonjwa kupata huduma bila ya kujali kwamba tunapunguza katika makusanyo yetu Serikali unataka tuwaangalie watu wetu jumuushi na maendeleo jumuushi bila kujali kwamba tunapunguza katika makusanyo yetu bila kujali wanalipia huduma au laa , nafurahi kwamba hamzuii wagonjwa kupata huduma   hilo ni jambo la kheri".

Ameutaka uongozi wa hospital hiyo kuwasiliana na uongozi wa Jiji la Tanga  kuweka mkakati wa pamoja katika kuhakikisha usalama wa afya kwa wananchi  wanaofika kupata huduma katika hospital hiyo unakuwepo wakati wote hii ikiwa ni njia ya kuendelea kuchukua tahadhari ya  kujikinga na mahonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindipindu  na homa ya nyani.

"Ni wajibu wa uongozi wa jiji la Tanga pamoja na hospital kuona hali nzima ya shughuli zinazoendelea nje ya hospital  kuweza na usimamizi nzuri pamoja na uwepo wa maji tiririka ili hospital iendelee kuwa katika mazingira mazuri kwa sababu katika hali ya sasa hivi hospital yetu ni chafu taka kila Kona ni lazima kuhakikisha kwamba mazingira ya hospital yetu ya nakuwa Bora na ya kuridhisha "

Awali akizungumza mganga mfawidhi wa hospital ya rufaa ya mkoa Bombo Frank Shega amesema kuwa ipo miradi mbalimbali inayotekelezwa katika hospital hiyo  ikiwemo ukarabati wa majengo ya kutolewa huduma ikiwemo  jengo la idara ya macho, jengo la mazoezi, jengo la kuhifadhia maiti , ambayo yote yanahitaji ukarabati kutokana naiundombinu yake kuwa ya muda mrefu.

Amesema pamoja na ujenzi wa majengo mbalimbali yanayojengwa ni pamoja na  jengo la damu salama ambalo litagharimu kiasi cha billion 2 linalojengwa kwa awamu mbili , mradi wa jengo la wodi binafsi ambao utagharimu shilingi Milion 199 ambapo tayari makandarasi ameshalipwa shilingi Milion 87 na ujenzi unaendelea.

"Fedha ambayo ilipitiahwa kwaajili ya ujenzi wa jengo la damu salama ni billion 2 ambalo litajengwa kwa awamu mbili n mradi wa jengo la wodi za binafsi maktaba wake ni Milion 199 na mpaka sasa mtaalamu ameshalipwa shilingi milion 87 bado tunaendelea kufanya malipo mengine kutokana na alipofikia"

Amesema kwa wastani  hospital hiyo imekuwa ikipokea wagonjwa wengi wa magonjwa yasiyoambukiza hususani shinikizo la juu la damu pamoja na kisukari wakifwatiwa na wagonjwa  wengine wakiwemo wa ajali.

Share To:

Post A Comment: