Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan ametembelea Makumbusho ya  Vita vya Majimaji iliyopo Mjini Songea Mkoani Ruvuma, kwa lengo la kutoa heshima ya Kumbukizi ya Mashujaa wa Vita ya MajiMaji vilivyopiganiwa takribani miaka 119 iliyopita .

Akiwa katika makumbusho hiyo iliyobeba historia ya kipekee Duniani,  Mhe. Rais Samia alipokelewa na viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii , wakiongozwa na  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana, Katibu Mkuu,Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, uongozi wa Mkoa wa Ruvuma , Chifu wa Wangoni Zulu Gama 1 , Wazee wa Mila na Desturi Mkoa  wa Ruvuma na Viongozi wa Dini.

Katika ziara hiyo. Rais Samia alitembelea Ukumbi wa Historia ya Vita ya Majimaji, onesho la Nyumba ya Inkosi( Chifu) wa Kabila la Wangoni pamoja na  kuweka Shada la Maua katika Kaburi la Halaiki la Mashujaa wa Vita ya Majimaji  na Kaburi la Chifu msaidizi( Nduna Songea Luwafu  Mbano.

Aidha, Mhe. Rais Samia ameweka  Silaha za jadi katika Mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa wa Vita ya Kagera.










Share To:

Post A Comment: