WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amewapongeza wanafunzi walioshinda katika mashindano ya wanasayansi vijana marufu Young Scientists Tanzania (YST) kwani yanasaidia kupata teknolojia ambazo zitatumika kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa   utoaji wa tuzo kwa washindi wa YST Profesa Mkumbo amesema kupitia mashindano hayo vijana wamekuwa wanatafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazokabili Jamii katika maisha ya kila siku.

"Kupitia mashindano haya  YST inaangalia kutafuta ufumbuzi wa kuangalia namna ya kutafuta  suluhisho kuhusu teknolojia kwa maisha ya baadae,"amesema Profesa Mkumbo.

Pia amesema hata tuzo ya YST Mwaka 2024 ni matokeo ya maendeleo ya utafiti  ya wanafunzi wa sekondari nchini kwa kuweka mawazo ya umakini wa kujituma katika Uhandisi wa teknolojia ya Sayansi na Hesabu nje  ya  maisha ya  darasani.
Aidha amesema kuwa matokeo hayo hayajatokea bila Serikali kuweka mikakati yake  katika uwekezaji wa shule za sekondari na kuendelea kuimarishwa kwa miundombinu ,rasiliamali watu  ili kupata matokea zaidi kwa baadae 
Hata hivyo amesema Taasisi ya YST imeweka mikakati kuisaidia Serikali  Kwa shule za Sekondari katika Sayansi ya Uhandisi wa Teknolojia pamoja na hesabu.




Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya YST,Profesa Yunus Mgaya amesema wanafunzi wamekuwa na mawazo ya kisayansi yenye kuwajenga  Kwa siku zijazo.







Share To:

Post A Comment: