Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla amewasili mkoani Arusha tayari kuanza ziara yake ya siku sita kwa Mkoa wa Arusha na Manyara.

Mwenezi Makalla amepokelewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Loy Sabaya pamoja na viongozi wa Chama Mkoa wa Arusha.

Makalla akiwa mkoani Arusha katika Wilaya za Longido,Monduli na Karatu tazungumza na wananchi kwenye mikutano ya nje,na kwamba na mikutano ya ndani yote ni kukagua uhai wa chama pamoja na kusikiliza kero za wananchi kisha kuzipatia majibu.

Aidha,baada ya kukamilisha ziara mkoani Arusha ataelekea Mkoa wa Manyara katika Wilaya za Babati na Simanjiro ambako pia atakuwa na mikutano ya ndani na nje kwa ajili ya kuwasikiliza wananchi na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM.










Share To:

Post A Comment: