Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amekabidhi computer mbili kwa ajili ya shule ya Msingi Ilemi Kata ya Iganzo Jijini Mbeya baada ya kuombwa ili kufanyia maandalizi ya mitihani.

Sanjari na na computer amekabidhi magodoro matatu kwa ajili ya watoto wenye uhitaji katika shule hiyo ili kupumzikia wakati wa masomo.

Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ndiye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya darasa la Saba chini ya Mwalimu Mkuu Sophia Malingumu ambapo watoto 182 wamehitimu.

Aidha ameahidi kutafuta Viti Mwendo Saba kwa ajili ya watoto wenye mahitaji Maalumu sanjari na kutafuta mashine ya kudurufia mitihani.








Share To:

Post A Comment: