Mwandishi Wa habari Godfrey Ng'omba Ripoter Wa Milady Ayo Arusha Leo amevamiwa na Askari polisi Kwa maelekezo ya mkuu Wa Mkoa Wa Arusha Paul Makonda  akiwa anarekodi tukio la watu kufunga Barabara ya Moduli kutokana na tukio la watoto wawili kupotea,polisi hao waliotaka kumpora camera alipo wazidi nguvu msaidizi mmoja Wa Makonda akashuka kwenye gari na kwenda kuwasaidia polisi akachoa Kadi ilivyokuwa kwenye camera yake na kuondoka nayo 


wananchi hao walifungwa Barabara kumzuia Makonda asipite akiwa anaetokea kwenye ziara yake Monduli Hadi wapate majibu ya kupotea Kwa watoto hao tukio Hilo limetokea maeneo ya Mbuyuni katika Kata ya Makuyuni wilayani Monduli


Inaelezwa kuwa Makonda baada ya kufika na Msafara wake alipomuona mwandishi huyo Wa habari akiwa na camera yake aliwaagiza Askari wamkamte na kuzuia habari hizo za watu kufunga Barabara zisionekane kwenye Chombo chochote Cha Habari.

Share To:

Post A Comment: