Msimamizi wa Uchaguzi wa
halmashauri ya Meru ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mwl.Zainab Makwinya leo ametoa maelekezo
ya kuongoza mchakato wa Uchaguzi kuanzia Uandikishaji wa Wapiga kura,uchukuaji
na urejeshaji wa fomu kwa Mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.
Maelekezo hayo yanatolewa siku 62 kabla yasiku ya uchaguzi wa serikali za mitaa kufanyika kwa lengo la kuhakikisha kuwa utaratibu unafuatwa na kwamba wapiga kura Pamoja na wagombea wanapata taarifa zote zinazohitajika kwa wakati.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika halmashauri hiyo Makwinya alisema kuwa fomu za kugombea zitatolewa na kutakiwa kurudishwa kuanzia tarehe moja hadi saba mwezi wa kumi na moja mwaka 2024, kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi.
Aidha maelekezo haya pia yanafafanua hatua zitakazoongoza
mchakato wa uchaguzi huo kuanzia uandikishaji wa wapiga kura,uchukuaji na
urejeshaji wa fomu za kugombea,uteuzi wa wagombea,kuhakikisha uchaguzi
unafanyika kwa uwazi,haki na sheria kwa
mujibu wa sheria na taratibu zilizopo.
Mwl.Zainabu alisema kuwa kwa mujibu wa kanuni ya 9 ya kanuni za uchaguzi wa mwenyekiti wa kijiji,wajumbe wa halmashauri
ya kijiji na mwenyekiti wa kitongoji katika mamlaka za wilaya za mwaka
2024,tangazo la serikali GN namba 571,la tarehe 12/7/2024 na kanuni za uchaguzi
katika mamlaka za miji midogo ya mwaka 2024 kupitia tangazo namba GN namba 572
ambazo zinatoa mwongozo mzima wa zoezi hilo la uchaguzi.
Alisema kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa utafanyika tarehe 27/11/2024,ambapo zoezi la uandikishaji wa wapiga kura litafanyika kuanzia tarehe 11 hadi 21 mwaka 2024 katika vituo vilivyopoangwa.
Pia ametia wito kwa ajili ya wakazi wote wenye umri kuanzia
miaka 18 na kuendelea waliokidhi
masharti ya kisheria wanaruhusiwa kushiriki katika uchaguzi huo,huku akiwataka wakazi wenye umri kuanzia miaka 21 au zaidi
kugombea nafasi ya uenyekiti wa Kijiji,ujumbe wa halmashauri ya Kijiji na enyekiti
wa kitogoji wanaruhusiwa kuchua fomu za kugombea fomu katika ofisi ya msimamizi
msaidizi wa uchaguzi.
Post A Comment: