Mdau wa maendeleo Mkoani Geita, ambaye pia ni Katibu wa Elimu, Malezi na Mazingira, Paschal Mapung'o, leo ametimiza ahadi yake kwa kikundi cha wanahabari cha Geita Media Group (GMG). Katika hafla hiyo, Mapung'o amekabidhi televisheni pamoja na kisimbuzi kwa kikundi hicho ambacho kinajihusisha na uandishi wa habari ndani ya Halmashauri ya Mji wa Geita.

 

Akiwa anakabidhi msaada huo, Mapung'o alieleza kuwa lengo ni kuwasaidia wanahabari wa GMG kuboresha shughuli zao za utoaji wa habari kwa umma kwa kuwa na nyenzo za kisasa. Aliwahimiza kuendelea kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maadili ya taaluma yao kwa maslahi ya jamii nzima ya Geita.

 

Kikundi cha GMG, kinachoongozwa na wanahabari wa eneo hilo, kilipongeza msaada huo na kusema kuwa ni chachu ya kuimarisha uwezo wao wa kutoa habari bora kwa jamii, hususan katika kueneza taarifa zinazohusu maendeleo ya mkoa wa Geita.

 

Msaada huu unatarajiwa kuboresha ushirikiano kati ya wadau wa maendeleo na wanahabari katika kuhakikisha taarifa sahihi na za uhakika zinawafikia wananchi kwa wakati.

 

 

Share To:

JOEL MADUKA

Post A Comment: