Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya na Mkurugenzi wa Maryprisca Women Empowerment Foundation (MWEF). 

Leo 27 Septemba, 2024 . Ametekeleza ahadi yake ya kuwasaidia wafungwa na mahabusu Gereza la Ruanda lililopo katika Jiji la Mbeya vifaa vya michezo mipira na seti mbili za sare pamoja na tank la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita elfu tano.

Aidha Mhe. Mahundi  ameahidi kwendelea kuwaunga mkono Kwa  kuwanunulia   magodoro  pamoja na ujenzi wa bweni kwa ajili ya wafungwa wanawake.

Kwa upande wake Mkuu wa Gereza la hilo Kamishina Msaidizi Sinjonjo Mwakyusa ameishukuru Taasisi ya Maryprisca Women Empowerment Foundation pamoja na Ofisi ya Mbunge  Mhe. Mahundi kwa msaada alioutoa  nakueleza kuwa utasaidia kuimarisha afya za wafungwa na mahabusu apo gerezani.


Share To:

Post A Comment: