Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe Omar Kipanga amewataka Wahandisi wa ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Bunda kuzingatia ubora wa kazi na ramani za majengo.

Kipanga amesema Chuo hicho cha Bunda ni miongoni mwa Vyuo 64 vinavyojengwa kwa kupitia agizo la Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha kila wilaya ya Tanzania bara inajengewa Chuo cha Ufundi na mafunzo ya udi stadi cha Wilaya

Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kukagua Maendeleo ya Ujenzi unaohusiha jumla ya majengo 18, ambapo tayari Serikali imeshatoa shillingi millioni 324.5 kwa ajili ya kazi hiyo.

"kukamilika kwa Chuo hiki kutasaidia kutoa Elimu ya ujuzi kwa wakazi wa wilaya hii na jirani utakao wawesesha kujiajiri na kuajiriwa ili baadae waweze kutimiza ndoto zao" alisema

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Bw. Hilary Majimbe amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza katika sekta ya Elimu na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kutekeleza maono ya serikali kwa vitendo katika kuandaa nguvu kazi yenye ujuzi.








Share To:

Post A Comment: