Mkuu wa Idara ya Utafiti kutoka Haki Elimu Makumba Mwemezi amesema utafiti uliofanywa na Taasisi hiyo umebaini kuwa asilimia 44.4 ya vijana katika shule za sekondari nchini hawana uelewa wa mambo gani yanayounda demokrasia huku asilimia 3.8 hawajui chochote kuhusu demokrasia.

"Kupitia utafiti huu tumegundua kuwa nchini Tanzania, elimu ya uraia ni sehemu ya mtaala wa shule, ambayo inalenga kuandaa wanafunzi wenye ufaulu wa juu kuliko kuwafundisha mchakato wa demokrasia" amesema Mwemezi na kuongeza

"Hata hivyo kuna wasiwasi mkubwa wa kupungua kwa vijana wanaoshiriki mchakato wa demokrasia kwani asilimia 29 ya wanafunzi wanakiri kuwa viongozi wa wanafunzi wanapatikana kwa kuteuliwa na walimu"

Mwenezi amesema Haki Elimu imeendesha programu ya Kivunge cha elimu ya uraia kwa shule za secondari kinacholenga kulea na kukuza ushiriki wa vijana Katika shughuli mbalimbali za kidemokrasia kuanzia darasani, shuleni hadi kwenye jamii.

Akichangia mada Katika mdahalo huo, mtoa mada Arif Fazel ambaye pia ni meneja mradi wa Action Aid amewataka vijana wenye nafasi ya kuwafikia vijana wenzao kufanya hivyo ili kuhakikisha kila kijana anakuwa sehemu ya utekelezaji wa maamuzi aliyoyapitisha.

"Mimi binafsi nimeshiriki katika michakato mbalimbali ya kidemokrasia, na hii inatokana na nafasi niliyonayo, sasa je ni vijana wangapi ambao wana nafasi kama yangu? Hivyo sisi wenye nafasi tutumie rasilimali ndogo tulizonazo kuhakikisha na wenzatu wanafikiwa? Alisema Fazel

Tumsume Vibweja kutoka Mbeya anasema vijana hawashirikishwi vya kutosha Katika michakato ya demokrasia akitolea mfano mchakato unaendelea wa kutoa maoni kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Taifa 2050.

"Sisi vijana hasa wa vijijini bado hatushirikishwi inavyotakiwa zaidi tunaletewa taarifa ambazo zimeshapitishwa, mfano halisi ni hili zoezi ya Dira ya Taifa, binafsi nimefanya jitihada kubwa sana kushiriki lakini licha ya kupata nafasi ya kushiriki lakini sikupata nafasi ya kutoa mawazo yangu" alisema Vibweja.



















Share To:

Post A Comment: